Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kubomoa nyumba 23 zilizojengwa kwenye mkondo wa mfereji kinyume na utaratibu ambazo zimesababisha maji ya mvua kushindwa kuingia kwenye mfereji mkuu unaopeleka maji baharini.
RC Shigela ametoa kauli hiyo baada ya Watu 119 kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Tanga.
MAFURIKO YALIVYOHARIBU NYUMBA ZAIDI YA 100 TANGA