Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya October 5, 2016 ni hii kutoka gazeti la Mwananchi yenye kichwa cha habari ‘Muziki tiba ya kukosa usingizi’
#MWANANCHI Utafiti wa chuo kikuu cha Tubingen Ujerumani umeonyesha Muziki wa taratibu ni msaada wa kuongeza uwezekano wa mtu kupata usingizi pic.twitter.com/xsav3q8BeF
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
Muziki ni tiba ya usingizi wakati wa usiku? Hilo ndilo swali ambalo wataalamu wengi huhangaika kupata majibu. Hata hivyo wakati juhudi za kutafuta tiba kwa wanaokosa usingizi usiku zikiendelea kupitia tafiti mbalimbali, Leo nakusogezea ushahidi wa kisayansi kuwa, Muziki husaidia kupunguza tatizo hilo.
Kwa mujibu wa utafiti, mtu asiyepata usingizi baada ya kupima afya yake na kuonekana hana tatizo lolote la kiafya, anashauriwa kutumia muda mwingi usiku kusikiliza muziki laini ili mishipa ya fahamu ifanye kazi vizuri.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Tubigeng cha Ujerumani, umeonesha kuwa muziki wa taratibu ni msaada wa kuongeza uwezekano wa mtu kuoata usingizi. Imeelezwa kuwa muziki husaidia kumfanya mtu anayetaka kulala kuimarisha kumbukumbu zake.
Kiongozi wa utafiti huo Dr. Jan Born anasema mtu anayesikiliza muziki wa aina hiyo hupata usingizi kwa urahisi tofauti na msikilizaji wa miziki mingine, hasa ile ya Hip Hop. Mtaalamu huyo anasema muziki huo huingia taratibu katika mishipa myembamba ya ubongo ambayo husaidia kufanya mwili wa binadamu na kupumzika kwa urahisi, hivyo kumrahisisha kulala.
Dr. Jan Born ameeleza kuwa Ubongo wa binadamu una mishipa isiyohitaji kelele ambayo hufurahi pale inaposikia sauti nyembamba au laini. Mishipa hiyo ndiyo huratibu mfumo mzima wa utulivu wa fahamu na wakati huo huo kurahisisha mawasiliano kati ya sehemu moja na nyingine ndani ya mwili katika mzaingira na hali ya utulivu, ili kuvifanya viungo muhimu vipumzike.
Ripoti ya Mtaalamu wa Saikolojia ambaye pia mkurugenzi wa taasisi ya Timamu Counseling, Anania Maulid anasema watanzania wengi wana tatizo la kukosa usingizi linalosababishwa na changamoto za kila siku za maisha.
Anania anasema hali iliyopo nchini haitofautiani na nchinnyingine zinazoendelea ambazo wananchi wake hufanya kazi katika viwanda vyenye mashine chakavu zinazotoa milio mikubwa ambayo huathiri mfumo wa usingizi kwa binadamu. Inaelezwa kuwa mtu anapofanya kazi katika mazingira yenye kelele, usingizi wake huwa wana kushtuka shtuka ambao huleta madhara.
Moja kati ya magonjwa yaliyotajwa kumpata mtu anafanya kazi kwenye makelele na kutopata usingizi ni pamoja na ugonjwa wa Moyo pamoja na Kiharusi ambacho huchangiwa na mtu kutopata usingizi mzuri, tatizo lililotajwa kukua kwa kasi zaidi nchini Tanzania.
Mtaalamu huyo wa masuala ya Saikolojia amesisitiza kuwa kuna ugumu katika kupata tiba ya moja kwa moja ya usingizi iwapo muhusika hana maradhi mengine yanayoambatana na suala hilo huku akiitaja Tanzania kuwa na waathirika wengi zaidi kuliko inavyodhaniwa.
#NIPASHE Waziri Mwakyembe amewaagiza DPP na DCI kufuatilia kikamilifu na kupeleleza ili kuwabaini waliohusika na mauaji ya watafiti Dodoma pic.twitter.com/S8Waid38Wi
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#NIPASHE Baada ya Muhimbili kudaiwa kutoza wajawazito wastani wa 300,000, Waziri Mwalimu ameitaka bodi kueleza sababu ya kuwalipisha pic.twitter.com/vCLFAX0ylJ
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#NIPASHE Rais Magufuli atangaza kumpatia bure Bakhresa zaidi ya hekta 10,000 za ardhi ili alime miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari pic.twitter.com/yqyqADueJA
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#HabariLEO Walimu wanafunzi wanne waliohusika kumpiga vibaya mwanafunzi Mbeya wafukuzwa chuo, wasubiriwa kupandishwa kortini pic.twitter.com/pJV2xtryxn
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#MWANANCHI Katika hali isiyo ya kawaida maelfu ya wanawake nchini Poland wameandamana kupinga muswada wa kuzuia utoaji mimba pic.twitter.com/EpZdNkKKew
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#MWANANCHI TAKUKURU yachunguza fedha za uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana ktk halmashauri ya wilaya ya Rombo mkoani K'njaro pic.twitter.com/TERgcPhhQH
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#MWANANCHI Wakazi wawili eneo la kivule DSM wauawa baada ya kutoka nje ya nyumba zao kutoa msaada kwa majirani waliokuwa wamevamiwa pic.twitter.com/tTM32HISRc
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#CHAMPION Imeelezwa kuwa mshahara wa kocha wa Taifa Boniface Mkwasa bado unalipasua kichwa shirikisho hilo kutokana na malimbikizo ya deni pic.twitter.com/sYPuhS83w6
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#MTANZANIA Watu milioni 14.1 duniani wanagundulika kuwa na saratani kila mwaka kati yao milioni 8.2 hufariki dunia pic.twitter.com/bEH6t5ucX5
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa kuwa zaidi ya 75% ya wanaume wamewakataa watoto wao, hali inayosababisha ongezeko la watoto wa mitaani DSM pic.twitter.com/LBMWBYTtCT
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#MTANZANIA Rais Magufuli amrudishia Bakhresa sukari yake iliyozuiwa bandarini kwa sababu biashara yake ina tija kwa taifa pic.twitter.com/wqSGgwHbsb
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016
#NIPASHE JPM ampa miezi miwili mtoto wa dada yake ambaye ni meneja TANESCO Pwani Martin Madulu kufikisha umeme kiwanda cha kusindika matunda pic.twitter.com/vsOtwaOej3
— millardayo (@millardayo) October 7, 2016