Watuhumiwa sita wanaodaiwa kumuua kwa makusudi aliekua Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dr. Sengondo Mvungi, wameachiwa huru katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kisha kukamatwa tena.
Waliachiwa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kuondoa shitaka hilo kwa kuwa hawana nia ya kuendelea nalo ambapo baada ya ombi hilo Washtakiwa wakaachiwa huru lakini wakakamatwa tena muda mfupi baadae na kupelekwa Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka mapya ya mauji ya Dr. Mvungi.
Washtakiwa ni Msigwa Matonya, Mianda Mlewa, Paulo Mdonondo, Longishu Losindo, Juma Kangungu na John Mayunga ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo November 3, 2013 maeneo ya Kibwerenge Msakuzi maeneo ya Mbezi Dar es salaam.
Walipofikishwa Kisutu wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mmbando na Wakili wa Serikali Lilian Rwetabura na kisha kesi ikaahirishwa hadi December 6, 2018.
NYOTA 3: MAISHA YA HASSAN NGARENARO, RAFIKI ZAKE 18 WAMEUWAWA KWA WIZI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA