Wakati mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam zikionekana tishio, hali imekuwa tofauti kwa Mtanzania James Mathias mkazi wa Tabata ambaye yeye amejitosa chini ya Daraja la Matumbi ili kuokota Makopo.
Camera za Ayo Tv zimemnasa James ambaye ni Baba wa Watoto wawili na mke mmoja, bila woga akiwa anaokota Chupa ili akauze apate rizki.
Mwandishi: James tumeona ukiingia chini ya daraja nini ambacho unakwenda kukitafuta
James: Ninaenda kuangalia chupa chupa hizi na kama hizi mbao unazoziona
Mwandishi: Lakini sio kwamba ni hatari kwako ?
James : Ni hatari lakini najitahidi kidogo kuw pembeni maan pembeni unapopaona ni mchanga.
“Chupa ninazookota inategemea na wingi wake maana Kilo moja ni shilingi mia tatu na zinauzwa kwa Kilo, kwa siku naweza kupata Kilo Kumi ama Kumi na Tano kama hivi hapa chupa zinakuja kwa wingi ndio unapata nyingi,”.