Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa iliyouita ni Hatarishi kwa Siku Tano ikionesha mikoa itakayoathirika zaidi ni iliyo katika Ukanda wa Pwani.
TMA imetoa angalizo la mvua kubwa siku ya Novemba 6, kwa baadhi ya mikoa ya Pwani na Ukanda wa Kaskazini katika mikoa ya Pwani, Dar na Tanga pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.
Aidha, hakuna tahadhari iliyotolewa katika siku za Novemba 07 na Novemba 08 ingawa Novemba 09 kumetolewa angalizo la mvua kubwa katika maeneo ya mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Pwani, Dar, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Hata hivyo, Mamlaka imebainisha kuwa uwezekano wa kutokea kwa utabiri huu ni wa Wastani na Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha Wastani.
Ikibainisha athari zinazoweza kutokea imesema ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za Kijamii na Kiuchumi.