Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Kati ya stori kubwa ambazo zimeandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii ya kwenye gazeti la Tanzania Daima yenye kichwa cha habari, ‘Wanafunzi wamng’oa meno matano mwalimu wao’
#TanzaniaDAIMA Wanafunzi Usevya sekondari Katavi wameshambulia walimu wawili wadai wanadhalilisha wanafunzi wa kiume pic.twitter.com/NciEoVYGjp
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
Wanafunzi kidato cha sita shule ya sekondari Usevya Halmashauri ya Mpwimbwe wilayani Mlele Katavi wamewacharaza viboko walimu wawili na kung’oa meno matano makamu mkuu wa shule hiyo, Makonda Ng’oka Membele.
Mwalimu mwingine aliyekumbana na kichapo hicho, Gabriel Kambona huku ikielezwa sababu za kuwapiga walimu hao ni kutokubali kufundishwa na mwalimu Membele kwa maaia kwamba ana tabia ya kuwadhalilisha wanafunzi wa kiume.
May mwaka huu mwalimu huyo alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpana kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake akidaiwa kutenda kosa hilo kati ya November mwaka jana na April mwka huu.
Inadaiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mwalimu Ng’oka kulitokana na wanafunzi hao kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi.
Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.
Hata hivyo baada ya kutopatikana kwa ushahidi wa kumtia hatiani mwalimu huyo, July 27 mwaka huu mahakama hiyo ilimuachia huru na August mosi alirudi kwenye kituo chake cha kazi ambapo iliwakera wanafunzi hao na kutaka mwalimu huyo aondoke.
Source: Tanzania Daima
#MWANANCHI TAKUKURU yamfukuza kazi mhasibu baada ya kubainika ana utajiri mkubwa, nyumba saba za ghorofa, viwanja 25 pic.twitter.com/6QOy3ZIELC
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#MWANANCHI Bunge laitaka Serikali kuleta majibu ya kuridhisha kuhusu hatua zilizochukuliwa baada ya tetemeko pic.twitter.com/ODDeZD0XR5
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#MWANANCHI Mchina, Mtanzania waunganishwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya bil 1.7 pic.twitter.com/cbqArlGj9w
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#MWANANCHI Serikali imeendelea kuupigia debe mji wa Dodoma na sasa imesema kuwa una vigezo vya kuwa jiji pic.twitter.com/YxXnu66TmK
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#HabariLEO RITA imezifuta taasisi 181 baada ya kushindwa kujitetea kwa nini zisifutwe pic.twitter.com/3IYiqQZKKo
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#HabariLEO Serikali imesema mipango iko mbioni kuzifanya manispaa za Moshi mkoani K'njaro na Dodoma kuwa majiji pic.twitter.com/fWMwP2dHdP
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#HabariLEO Serikali ya Tanzania inafikiria kufungua ubalozi wake nchini Sudan Kusini hali ya kifedha itakaporuhusu pic.twitter.com/55ixUGNsN4
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#HabariLEO Madaktari, matabibu na wauguzi ndio wanaoongoza kwa mishahara mikubwa ikilinganishwa na sekta nyingine pic.twitter.com/MbCEBh38me
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
MTANZANIA Jamhuri yapinga hoja za mke bilionea Msuya kuwa waliteswa ili wakili kumuua dada wa bilionea huyo pic.twitter.com/imdtvSTsM9
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#MTANZANIA Wakurugenzi waombwa kuacha kufanya kazi kwa mitandao kwa kuwa imekuwa ikitoa habari ambazo sio sahihi pic.twitter.com/0whcA29S05
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#JamboLEO Hatma ya uenyekiti wa Lipumba CUF mikononi mwa Msajili kutokana na ofisi hiyo kuzikutanisha pande mbili pic.twitter.com/1djDT0h9x9
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#NIPASHE Mbunge Gulamali atoboa wabunge wanavyoongwa, asema aliambiwa hiki kipindi kibaya pesa za rushwa zimepungua pic.twitter.com/DuwdaEdXyz
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
#NIPASHE Wakati Serikali ikichangia bil 1.4 walioathirika na tetemeko, imeelezwa zinahitaji zaidi ya bil 2.3 pic.twitter.com/yKFJGFMSKk
— millardayo (@millardayo) September 14, 2016
ULIKOSA UFAFANUZI KUHUSU VIPIMO VYA MATETEMEKO YA ARDHI VILIVYOIBIWA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI