WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukuwa sampuli za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Waziri Mkuu amesema wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo una kiasi gani cha dhahabu pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.
Waziri Mkuu amechukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa,”-Waziri Mkuu, Majaliwa
VIDEO: Rais Magufuli alivyoipokea ripoti ya CAG na kutoa maagizo, Bonyeza play hapa chini kuitazama