Wakati takwimu za Shirika la Afya Dunia (WHO) zinakadiria watu zaidi ya 3,400 hupoteza maisha kila siku kwa ajali za barabarani, Jeshi la Polisi nchini limesema kwa mwaka 2020 limefanikiwa kupunguza ajali kwa asilimia 33.
Akizungumza, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, amesema Januari hadi Novemba mwaka jana 2019 ajali zilizosababisha vifo ni 1,117 huku waliopoteza maisha 1,329 na majeruhi ni 2,717.
Amesema Januari hadi Novemba mwaka huu wa 2020, jumla ya matukio ya ajali ni 1,800 ajali zilizosababisha vifo ni 935, waliofariki ni 1,158 na majeruhi ni 2,089.
“WATOTO WAMETOROKA SHULE WAMEJIUNGA NA VIKUNDI VYA KIHALIFU” SABAS