Hiroshima, mji wa Japan ulioharibiwa na bomu la atomiki la Marekani mwaka 1945, uko katikati ya mzozo unaoongezeka baada ya maafisa wa eneo hilo kutupilia mbali wito wa kuiondoa Israel katika sherehe zake za kila mwaka za kuhimiza amani duniani huku vita vikiendelea huko Gaza.
Kila mwaka mnamo Agosti 6, Hiroshima hukusanya maafisa wa kigeni, pamoja na wenyeji, katika dakika ya kimya saa 8:15 asubuhi kuashiria wakati kamili wa kurushwa kwa bomu, na kuua makumi ya maelfu ya watu na kusababisha mwisho wa Vita vya Kidunia vya pili.
Baadhi ya wanaharakati na makundi ya walionusurika kwenye bomu la atomiki wanasema sherehe hiyo sio mahali pa Israel, ambayo inaishambulia Gaza kwa lengo la kutokomeza Hamas kujibu mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Palestina Oktoba 7 mwaka jana.
Wanasema serikali ya mji wa Hiroshima inapaswa kuiondoa Israel katika sherehe za mwaka huu, kwani ina Urusi na Belarus kwa miaka miwili iliyopita kutokana na uvamizi wa Moscow nchini Ukraine.
Lakini mamlaka ya Hiroshima inasema hawana nia ya kuitenga Israel.