Serikali mkoani Mbeya, imelaani vikali mauaji ya Mwalimu Hemed Mwaipopo (54) wa shule ya Msingi Mwenge wilaya ya Kyela anaedaiwa kuchinjwa shingoni na watu wasiojulikana na kisha mwili wake kutelekezwa pembezoni mwa barabara kuu ya Ipinda Matema wilayani humo.
Mwalimu Mwaipopo alikuwa mkazi wa Kitongoji cha Mpanga Kijiji cha Mpunguti Kata ya Ikama anasadikika kuchinjwa na watu wasiojulikana kwa sababu za mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya marehemu na familia iliyomuuzia eneo alilojenga nyumba yake.