Mwalimu Yusuph Pangoma ni mmoja ya walimu waliopata umaarufu nchini kwa mfumo wake wa kufundisha wanafunzi wake akiwa anacheza mziki na michezo mbali lakini muda huohuo akiwafundisha wanafunzi hao na kuelewa vizuri.
AyoTV imempata mwalimu huyo akiwa likizo Wilaya ya Temeke akifundisha Shule ya Msingi Mbagala kuu kwa kujitolea kuwanoa wanafunzi wa darasa la saba masomo ya sayansi licha yeye kuwa mwajiliwa katika shule ya msingi Wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara.