Mwanafunzi mmoja amefariki dunia huku wengine saba wakiwa hawajulikani walipo na watu wengine watatu kukimbizwa hospitali baada ya gari ya shule ya Ghati Memorial kutumbukia mtoni majira ya asubuhi katika kata ya Sinoni Mkoani Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amesema wanamshikilia dereva wa gari hiyo huku chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni dereva huyo kulazimisha kupita.