Mwanafunzi Gift Lema aliyekuwa akisoma katika shule ya Sekondari Ritaliza,iliyopo katika Kata ya Holili,Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro aliyetoroka kwa kuchora ramani iliyokuwa inaonyesha anataka kwenda marekani amepatikana mpakani mwa Tanzania na Kenya huku akidai kwamba lengo la kuondoka na kutokana na Tanzania kufundishana masomo Mengi tofauti na Marekani na kwamba anakoenda atakuwa huru zaidi
Meneja wa shule hiyo amesema Mwanafunzi huyo aliyetoroka siku kumi zilizopita amepatikana na alipoondoka alikuwa na shilingi elfu nane tu lakini awali alichora ramani iliyokuwa ikionyesha mazingira ya shule hadi pale atakapofikia kwa maana ya USA