Erick Laizer ni mwanafunzi mtanzania anayesoma chuo cha African Leadership Academy kilichopo South Africa, alipata nafasi hiyo baada yakugundua mtambo wakumsaidia mtu kujilinda na majanga mbalimbali ikiwemo moto,wizi na hitilafu za umeme ambapo aliibuka nakushika nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya kisayansi. Tanzania
Erick anasema kwenye chuo anachosoma cha African Leadership Academy analipwa zaidi ya laki mbili kwa siku kwa kutengeneza vifaa mbalimbali kama simu laptop ukiachia mbali fedha nyingine anazolipwa na wanafunzi wenzake kwa kuwatengenezea vifaa mbalimbali na fedha ambayo ameikusanya amewajengea wazazi wake nyumba ya shilingi millioni 40.