Patricia Cardozo ni mkurugenzi wa NGO ya haki za wanawake iitwayo Plataforma Feminista Boyacense (Boyacense Feminist Platform), ambayo inafanya kazi kukomesha unyanyasaji nyumbani, unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi, ikiwa ni pamoja na kuwaokoa waathiriwa kutoka kwa mikono ya wanyanyasaji ambapo siku ya Jumatatu, mshambuliaji asiyejulikana alimrushia kilichosemekana kuwa tindikali alipokuwa akitembea kwenye bustani.
Polisi wa Colombia bado wanachunguza shambulio hilo lililotekelezwa dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu, Lilia Patricia Cardozo, katika eneo la kaskazini-magharibi la Boyaca nchini humo ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa kimatibabu, alipata majeraha katika sehemu ya kushoto ya uso wake, msemaji wa NGO hiyo aliandika kwenye Facebook.
Hospitali ya Chuo Kikuu cha San Rafael de Tunja ilisema kemikali aliyo mwagiwa Cardozo iliathiri 4% ya mwili wake, ikiwa ni pamoja na uso wake, na kifua chake.
Cardozo amekuwa mlengwa wa vitisho vya kuuawa tangu 2022, ambayo ilisababisha Kitengo cha Ulinzi polisi wa nchi hiyo kuidhinisha itifaki ya usalama ya kumlinda Septemba mwaka jana..
Jukwaa la Wanawake wa Boyacense limeshutumu mamlaka za eneo la Tunja kwa kutompa ulinzi wa kutosha Cardozo
Wanawake na watetezi wa haki za binadamu wako hatarini hasa nchini Kolombia. Mnamo 2022, kesi 614 za mauaji ya wanawake ziliripotiwa, kulingana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Colombia.
Tangu mwaka 2016, zaidi ya wanaharakati 500 wa haki za binadamu wameuawa nchini humo, na kuifanya kuwa moja ya nchi hatari zaidi kwa watetezi wa haki za binadamu duniani kote, kulingana na Human Rights Watch.