Mwanamitindo Mtanzania Flaviana Matata ameeleza kufurahishwa na ukweli aliouzungumza Mwimbaji Staa wa Uingereza Adele kwenye Interview na Oprah ambapo amefunguka kuhusu maisha yake na kuvunjika kwa ndoa yake.
“Nilipenda sana uaminifu wa Adele kwenye mahojiano yake na Oprah kuhusu maisha yake na talaka, kabla ya kuaibisha Watu kuhusu talaka tafadhali jaribu kuwa na huruma, hakuna Mtu anayeolewa ili apate talaka, nikiongea kwa uzoefu wangu wa binafsi nilitalikiana mwaka 2019 na mtandao haukuniruhusu kupumua, ilikuwa kana kwamba nimeua Mtu”- Flaviana Matata
“Niko katika nafasi nzuri sana kwa sasa na ninajiona nimepona, asante kwa Watu wangu kwa kuwa pale kwa ajili yangu kwani ilikuwa ya kikatili kweli, ni kwamba baadhi yetu huchagua kuficha maumivu mbele za umma, Mtandao unaweza kuwa wa kikatili sana na hii ndiyo sababu ni vigumu kwa Watu kufunguka kuhusu mapambano yao isipokuwa wale wachache wenye ujasiri”- Flaviana Matata
“Hatusaidii Mtu kwa kumuaibisha Mtu wakati ndoa haifanikiwi na hii ndiyo sababu ya Watu kukaa kwenye ndoa zenye huzuni, matusi na sumu, mahojiano ya Adele yalinigusa sana na yamenitia moyo hatimaye kusema kitu, tunahitaji kufanya vizuri, Mungu ni upendo, kwa ufupi… Jamii yetu inapaswa kufanya vizuri zaidi na kuacha kuwalaumu Wanawake wakati ndoa hazifanyiki na kwanini Wanawake ndio wa kulaumiwa??”– Flaviana Matata