Naomi Campbell amekiri kwamba alikuwa “akijaribukujiua” kwa kutumia dawa za kulevya katika miaka ya 90 alipokuwa kweny mahojiano kuhusu kupambana na uraibu katika maisha yake .
Mwanamitindo huyo na star mzaliwa wa Brit, ambaye ametumia muda mwingi wa maisha yake akiishi New York, alikiri kuwa aligeukia Cokeini na pombe kama njia ya kushughulikia maswala ya kutelekezwa utotoni alipojidhihirisha katika mahojiano ya filamu mpya ya AppleTV+, The Super Models.
Pia alifichua kuwa uraibu wake ulichochewa na huzuni aliyopata kufuatia mauaji ya rafiki yake wa karibu na mbunifu mashuhuri Gianni Versace.
Ulimwengu wa mitindo ulitikiswa wakati mwanadada huyo wa Italia alipouawa nje ya nyumba yake Miami Beach mnamo 1997 na Naomi alijitahidi kustahimili kifo chake.
Akielezea uhusiano wao wa karibu, alisema: “Alikuwa mtu muhimu sana kunifanya nifanye maisha yangu bora alinisukuma kwenye kazi yangu hii. Alikuwa akinisukuma nitoke nje na kwenda mbali zaidi wakati wakati huo sikufikiria kwamba nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo na alikufa, huzuni yangu ikawa mbaya sana.”