Mwanamke tajiri na mama wa watoto watatu, Jennifer Gledhill (42), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumpiga risasi mumewe hadi kufa akiwa amelala baada ya ugomvi mkali kuhusu madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.
Mama huyo anadaiwa kumuua mume wake, Matthew Johnsonn(51), aliyekuwa mwanachama wa Kikosi cha Kitaifa cha Utah ndani ya nyumba yao iliyopo Cottonwood Heights mwishoni mwa Septemba, baada ya mume wake kugundua alikuwa amelala na mtu mwingine siku moja kabla, ambapo Gledhill alikiri kufanya hivyo kwa mujibu wa wachunguzi.
Baada ya mauaji hayo, mama huyo anadaiwa kuutupa mwili wa mume wake kisha kuripoti kupotea kwake mnamo Septemba 28, siku nane baada ya mauaji hayo.
Hata hivyo, mauaji hayo yalifichuliwa baada ya mwanaume mmoja kujitokeza na kuwaambia polisi kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Gledhill, na kwamba alikiri kwake kuhusu mauaji hayo ya kutisha.
Gledhill alidaiwa kusafirisha mwili wa mume wake kuelekea kaskazini, akachimba shimo, na kumzika kwenye kaburi la kina kifupi. Ili kuficha ushahidi, anadaiwa kuvunja simu ya Johnson, na kuendesha gari lake hadi eneo lingine la mtaa, na kisha kulisha gari lake kwenye kituo cha kuoshea magari.