Mkazi wa Tabata Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, Mariam Mwakabungu (25) ambaye ni Mke na Mama wa Watoto wawili amejitolea (Bila kulipwa) kuokoa maisha ya Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) na kisha kutelekezwa na Mama zao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ambapo mpaka sasa amesadia Watoto watatu kwa kuwakumbatia kwa siku nzima ili wapate joto linalowasaidi kuongeza uzito wao.
@AyoTV_ imefanya mahojiano maalum na Mariam ambapo amesema alianza kutoa huduna hiyo baada ya kumtembelea Rafiki yake aliyejifungua Mtoto njiti na kumuona Mtoto ambaye alishi kwa muda wa miezi minne bila kuongezeka uzito na akaguswa zaidi kwakuwa yeye Mariam ni Yatima ambaye hakupata bahati ya kulelewa na Wazazi hivyo akaona hilo ni jukumu lake.
Mariam halipwi chochote zaidi ya Manesi kumchangia fedha ya chakula na kwa sasa ana zaidi ya Mwezi mzima anaishi Hospitali akifanya huduma hiyo “Mume wangu ni muelewa hana shida Mimi kuishi Hospitali, Mtoto wa kwanza nilimuhudumia Wiki moja kwa Mume wangu haikuwa shida lakini Mtoto wa pili nilikaa Miezi miwili hapo Mume wangu kidogo akapiga simu mbona hii umechelewa sana, huyu ni Mtoto watatu”
Namba za kumpa support Mariam kwa kazi nzuri anayoifanya ni 0782124700 (Alise Mwakabungu)