Ni muendelezo wa story ya Mwanamke wa Uganda, Ann Grace Aguti(36) ambaye amewaoa Wanaume watatu na kumpa kila mmoja wao nyumba moja kati ya Saba anazomiliki, unaambiwa walikuwa Wanaume wanne lakini mmoja akatimuliwa na Ann Grace kwakuwa alizidisha wivu na kutaka Mwanamke alale na yeye tu kila siku.
Ann ndie kichwa cha Familia, Wanaume wanatii maamuzi yake na amejipangia mzunguko wa ratiba ya kulala kwenye kila nyumba ya Mwanaume wake, ila bado ndoto yake ni kumpata Mwanaume wa nne atakayemuhudumia kama anavyowahudumia Wanaume.