Venna Mushi ni Mwanamke ambaye video zake zimesambaa akidaiwa kufumaniwa na Mume wa Mtu, amezungumza na kusema hakufumaniwa ndani ya nyumba kama ilivyodaiwa bali alikuwa amesimama nje na Mwanaume huyo wakiwa wanajadili masuala ya biashara.
Venna amedai alichukuliwa fedha zake zaidi ya Tsh.Laki tisa na Mwanamke huyo aliyempiga, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mgwhira amefika nyumbani kwa Mwanamke huyo na kusema atahakikisha anapata matibabu na taratibu nyingine za kisheria zitafuata.