Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 31 Dorcas Jepkemoi Chumba aliteleza na kuzama kwenye maporomoko ya maji ya Chepkiit katika Jimbo la Nandi, wakati akipiga picha.
Mchumba wake Dorcas, Benjamin Kazungu amesema walikwenda kwenye maporomoko kupumzika wakati wa mchana, safari ambayo walikuwa wameipanga kwa muda mrefu.
Picha alizokuwa akipigwa na mchumba wake zilikuwa ndio picha za mwisho kwenye kumbukumbu yake, Kazungu ameeleza jinsi mchumba wake alivyokuwa anapendeza wakati akipiga picha na jinsi alivyoteleza kwa bahati mbaya kabla ya kuteleza na kutumbukia kwenye bwawa lililofurika na kutoweka majini.
Familia ya mwanadada huyo iliweka kambi kwenye maporomoko hayo ikitumaini kwamba mwili wake utapatikana, lakini jitihada zote za wapiga mbizi hazikufanikiwa.