Katika Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, tarehe 25 Novemba, ripoti ya Femicides mwaka 2023: Makadirio ya Kimataifa ya Mauaji ya walio kwenye mahusiano / UN Women na UNODC inafichua kuwa mauaji ya wanawake imekuwa aina kali zaidi ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na imesalia kuenea duniani kote.
Mahali pa hatari zaidi kwa wanawake ni nyumbani na wanawake na wasichana 140 kwa wastani waliuawa na wenza wao wa karibu au mwanafamilia kwa siku mwaka jana, mashirika hayo mawili ya Umoja wa Mataifa yaliripoti Jumatatu.
Ulimwenguni, mshirika wa karibu au mwanafamilia alihusika na vifo vya takriban wanawake na wasichana 51,100 wakati wa 2023, ongezeko kutoka kwa wastani wa wahasiriwa 48,800 mnamo 2022, UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu ilisema.
Ripoti hiyo iliyotolewa katika Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake imesema ongezeko hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na takwimu nyingi zaidi kutoka katika mataifa
Lakini mashirika hayo mawili yalisisitiza kuwa “Wanawake na wasichana kila mahali wanaendelea kuathiriwa na aina hii ya ukatili wa kijinsia uliokithiri na hakuna eneo ambalo limetengwa.” Na walisema, “nyumbani ni mahali pa hatari zaidi kwa wanawake na wasichana.”
Idadi kubwa zaidi ya mauaji ya wenzi wa karibu na familia ilikuwa barani Afrika – na wastani wa wahasiriwa 21,700 mnamo 2023, ripoti ilisema. Afŕika pia ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya wahasiriwa ikilinganishwa na ukubwa wa wakazi wake wahasiriwa 2.9 kwa kila watu 100,000.