Mwanamke wa Marekani aliye na mifuko miwili ya uzazi amejifungua mara mbili ndani ya siku mbili.
Kelsey Hatcher, 32, alijifungua mtoto wa kwanza siku ya Jumanne, na wa pili Jumatano, katika Hospitali ya Birmingham (UAB) ya Chuo Kikuu cha Alabama.
Akitangaza kuwasili kwa “watoto wake wa ajabu” kwenye mitandao ya kijamii, Bi Hatcher aliwasifu matabibu hao kuwa “wa ajabu”.
Watoto hao wakike wanasemekana kuwa mapacha nadra – ingawa walizaliwa siku tofauti.
Mama huyo alifahamishwa kuwa ana mifuko miwili ya uzazi akiwa na umri wa miaka 17 – tatizo nadra ambayo UAB ilielezea kuwa ya kuzaliwa inayoathiri 0.3% ya wanawake.
Uwezekano wa kupata ujauzito katika uterasi – mimba ya dicavitary – ilikuwa ndogo zaidi, “moja kati ya milioni”, kulingana na UAB.
Visa vilivyoripotiwa kote duniani ni vichache sana.
Mnamo mwaka wa 2019, daktari mmoja nchini Bangladesh aliambia BBC kuwa mwanamke mmoja alikuwa amejifungua mapacha mwezi mmoja baada ya kujifungua mtoto njiti.