Katika tukio la kutatanisha kutoka Brazili, mwanamke alileta maiti ya mwanamume mwenye umri wa miaka 68 kwenye kiti cha magurudumu ndani ya benki ili kumtumia yeye kusaini barua ya mkopo, walisema polisi, Jumatano (Aprili 17).
Erika de Souza Vieira Nunes alimkalisha mwanamume huyo ambaye alimtaja mara kwa mara kama “mjomba” – hadi kwenye benki katika kitongoji cha Rio wakati wafanyakazi walihisi kuwa kuna kitu hakiko sawa.
Siku ya Jumanne (Aprili 16), Nunes aliipeleka maiti kwenye benki huko Rio na kumwambia muhudumu wa benki kwamba mzee huyo alitaka mkopo wa $3,250.
Katika picha ya kamera ya usalama, Nunes alionekana amesimama karibu na marehemu ambaye alikuwa kwenye kiti cha magurudumu na mwanamke huyo akionekana kujaribu kuinua kichwa cha mtu huyo kilichoinama mara kwa mara.
Baadaye, alionekana akizungumza na aliyekuwa akimuhudumia na hata kushikilia kalamu na kusogeza mkono wake mbele bila majibu.
Katika picha za kutatanisha zilizorushwa kwa mara ya kwanza huko Brazil, Nunes alionekana akiitaja maiti kama “mjomba” wake, na kumtaka atie saini hati za kifedha ambazo zingemruhusu kuchukua mkopo.
“Mjomba unasikiliza? Unahitaji kusaini. Usipotia saini, hakuna njia, kwa sababu siwezi kukusainia,” anasikika akisema kwenye video za usalama, akimtaka atie saini hati hizo.
Aliongeza, “Saini ili usinitie maumivu ya kichwa tena, siwezi kuvumilia tena.”
alipo ulizwa kwanini mjomba wake hajibu alisema “Hasemi chochote, ndivyo alivyo,” alisema, na kuongeza, “Ikiwa hauko sawa, nitakupeleka hospitalini.”
Walakini, wafanyikazi wa benki hawakuamini hadithi yake kwani tayari walikuwa na mashaka na kuwaita polisi ambao walimkamata Nunes papo hapo.
Wakati huo huo, maiti hiyo iliripotiwa kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.