Jopo la Majaji katika Jiji la Houston Marekani limeamua kwamba Mwanamke aliyetajwa kwa herufi za kwanza za D.L atapokea dola bilioni 1.2 kama fidia kutoka kwa Mpenzi wake wa zamani ambaye alisambaza picha zenye maudhui ya ngono kwenye mitandao ya kijamii bila ridhaa yake.
Habari hii inakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya Mwanamke huyo April 2022 kuwasilisha kesi ya unyanyasaji dhidi ya Ex wake huyo aitwae Marques Jamal Jackson, kwa kudukua computer yake binafsi na kuiba picha zake kisha kuzipost mitandaoni.
Mwanamke huyo anasema Jackson alianza kumtishia maisha na kumsumbua baada ya kuvunja penzi lao la miaka minne mwaka 2020 ambapo Mshtakiwa anadaiwa ku-post picha za Mwathiriwa kwenye mtandao wa Facebook, Twitter, Dropbox na hata Pornhub na kuzituma picha hizo kwa marafiki na familia ya D.L. kupitia email.
Jumla ya pesa ambazo Mwanamke huyo anatakiwa kulipwa na mahakama inajumuisha dola milioni 200 kutokana na mfadhaiko wa akili aliopitia kwa sasa na miaka ijayo pamoja na $1 bilioni kutokana na uharibifu uliosababishwa na maudhui hayo kwenye maisha ya Mwanamke huyo.