Kutokea nchini Marekani, moja kati ya habari kubwa no kuhusu hukumu ya miaka 30 Jela dhidi ya Mwanamuziki Robert Sylvester Kelly maarudu kama R.Kelly.
R.Kelly amehukumiwa June 29, 2022 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono mbele ya Jaji Ann Donnelly baada ya kukubaliana na hoja za upande wa mashitaka.
Katika hukumu hiyo ya kihistoria katika sekta ya Muziki, Jaji Ann alisikika akisema “umma lazima ulindwe dhidi ya tabia mbaya kama hizi”
Hukumu ya R.Kelly inakuja ikiwa ni takribani miezi 10 baada ya kupatikana na hatia katika mahakama ya shirikisho ya Brooklyn, N.Y. Septemba 2021.
Hukumu hiyo inajiri miaka 14 baada ya Kelly kuondolewa mashtaka 14 katika kesi ya ponografia ya watoto huko Illinois. Kelly pia anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ngono katika jimbo la nyumbani la Illinois na Minnesota.
Awali waendesha mashtaka walimuomba Jaji kumuhukumu R.Kelly kifungo kisichopungua miaka 25 jela, umhukumu Kelly, 55, kifungo cha zaidi ya miaka 25 jela.
R.Kelly alikamatwa mwaka 2019 dhidi ya tuhuma hizo ambapo alifikishwa mahakamani, huku moja kati ya vitu vilivyoelezwa ni kwamba alimuoa Aaliyah aliyekuwa na miaka 15.