Jana nilikusogezea stori kutoka hospitali ya Mwananyamala kuhusu kupokea idadi ya wagonjwa wa kipindupindu 20 na kufariki kwa watu watatu, sasa leo ripota wa millardayo.com amefika tena hospitalini hapo kuhakikisha kinachoendelea Hospitalini hapo.
Taarifa kutoka hospitali ya Mwananyamala ni kwamba leo wameshapokea wagonjwa 8 ambao wanahisiwa kuwa na vimelea vya ugonjwa huo wa Kipindupindu.
‘Hali ya leo jana walikuwa 20 kwa hiyo leo wakaongezeka tena 8 kwa hiyo jumla tuna wagonjwa 28 kati ya wagonjwa hao wagonjwa 9 wamepata nafuu tumewaruhusu kwenda majumbani kwao na wagonjwa wengine 5 tumewapeleka katika kambi ya kipindupindu Mburahati na wengine 5 majibu yao yanaonesha (positive) kuwa wanavimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kwa hiyo nao tunatakiwa leo hii kuwapelekea nao Mburahati’ – Dk Ngonyani
‘Na waliobaki 8 bado tunao katika hospitali yetu ya Mwananyamala wanaendelea na uchunguzi na matibabu hakuna mgonjwa yoyote aliyefariki siku ya leo‘ – Dkt. Ngonyani.
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Dkt.Ngonyani
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos