Mwanariadha wa Kenya, Kelvin Kiptum amekuwa mwanaume wa kwanza kukimbia mbio za marathon kwa kutumia saa 2 na sekundi 35, na kuweka rekodi mpya ya dunia katika Mbio za Marathon za Chicago zilizofanyika jana jumapili.
Kiptum alivunja rekodi iliyowekwa na mwanariadha mwenzake wa Kenya, Eliud Kipchoge katika mbio za mwaka jana za Berlin.
Hii ni mara ya tatu kwa wanaume kuweka rekodi katika mbio za Marathon za Chicago, ambapo rekodi ya kwanza iliwekwa na mkimbiaji Khalid Khannouchi wa Morocco mwaka 1999.
“”I knew I was coming for a course record, but a world record – I am so happy,” Kiptum said. “A world record was not on my mind today, but I knew one day I would be a world record-holder.”
Kiptum alisema. “Rekodi ya dunia haikuwa akilini mwangu leo, lakini nilijua siku moja nitakuwa mmiliki wa rekodi ya dunia.”
Kipchoge pia alivunja mwendo wa saa 2 mwaka wa 2019 katika maonyesho maalum ya Vienna ambayo hayafuzu kwa rekodi ya dunia.
Hassan ni wa pili nyuma ya rekodi ya dunia ya wanawake ya saa 2:11:53 iliyowekwa mwezi uliopita mjini Berlin na Tigist Assefa wa Ethiopia. Assefa alivunja rekodi ya dunia ya wanawake kwa zaidi ya dakika mbili.