James Verone wa North Carolina, Marekani alivamia Bank mwaka 2011 na kumuamuru Muhudumu wa Bank ampe dola moja ya kimarekani (Tsh. 2319 leo) kwa lazima lengo lake likiwa ni kutaka Polisi wamkamate aende Jela ili apate matibabu kiurahisi.
“Sikuwa na Bima ya Afya matibabu yakawa shida, nashukuru nipo Gerezani natibiwa vizuri tena bure na kila ninapohitaji kuonana na Daktari naonana nae, naamini hadi kifungo kikiisha nitakuwa nimepona”
Verone ambaye kwa sasa umri wake ni miaka 68 alikua akifanya kazi mbalimbali ikiwemo ya Udereva wa Lori lakini aliachishwa kazi hiyo na kurudi mtaani ambapo mambo yalipokua magumu ndio ikabidi abuni njia hiyo ya kufanya kosa la makusudi ili apelekwe jela wakati akiwa na miaka 59.
Anasema alivamia Benki kwa makusudi ili afungwe jela miaka mitatu ili atumie hicho kipindi kupata matibabu ya vilivyokua vinamsumbua mwilini ambapo alihitaji kufanyiwa upasuaji wa mgongo, kutibiwa maumivu mguuni na kifuani ambapo wakati ameshikiliwa na Polisi alitoa kauli nyingine kwamba kama atapewa kifungo kifupi gerezani basi atakwenda kuiba tena ili afungwe amalizie matibabu yake vizuri.
Unaambiwa siku ya kwenda kuiba Benki, baada ya kuamuru apewe hiyo dola moja ya kimarekani alisogea na kwenda kukaa kwenye kochi ndani ya Benki hiyo na kuwasubiria Polisi waje kumkamata, baada ya kukamatwa alisema pia kwamba “ninachohitaji ni kutibiwa, kama huna afya, hauna chochote kwenye hii dunia”