Mwanaume mmoja Abiria wa Ndege ambae jina lake halijafahamika amesifiwa kwa upendo na kujali kwa hali ya juu baada ya kusimama kwenye Ndege kwa dakika 360 (saa 6) ili tu kumpisha Mke wake alale kwa kujinyoosha kwenye viti.
Tunafahamu jinsi viti vya daraja la ‘economy’ kwenye Ndege vinavyokua vidunchu hata ukisema ujilaze kwenye kiti kimoja panakua pamebana sana, Mwanaume huyu aliamua kuondoka kwenye kiti chake na kusimama ili angalau Mke wake apate eneo kubwa zaidi la kujilaza kwa kunyoosha miguu.
Picha hii ilipigwa na Abiria mwenzao aliyekua pembeni ambaye alionekana kufurahia kitendo hicho na kuandika “Huu ndio upendo” ambapo pamoja na wengine kuona huu ni upendo wa hali ya juu, wengine mitandaoni wamekosoa na kusema labda kama Mwanamke alikua Mgonjwa ila kama hakuwa Mgonjwa basi amefanya kosa na atakua ni Mwanamke Mbinafsi.
Je hapo ulipo umewahi kumpisha wapi au kumpa nafasi Mpenzi wako hata kama sio kwenye Ndege?