Polisi wa Uhispania wamemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumnyanyasa kingono mwandishi wa habari baada ya kudaiwa kumgusa alipokuwa kwenye TV.
Isa Balado alikuwa akiripoti kuhusu wizi siku ya Jumanne huko Madrid wakati mwanamume mmoja alipomwendea kwa nyuma na kumpapasa kabla ya kuuliza ni kituo gani anachofanyia kazi.
Balado alimfata na kumkabili kijana huyo na kumueleza kuwa alikuwa akifanya kazi na kujaribu kuendelea na ripoti yake, lakini mtangazaji mwenzie Nacho Abad alisisitiza kwamba aonyeshe uso wa mwanamume huyo kwenye kamera.
Polisi walisema katika ujumbe kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulikuwa wa Twitter, kwamba mwanamume mmoja alikamatwa Jumanne kwa kumnyanyasa kingono mwandishi.
Tukio hili linakuja huku kukiwa na mzozo wa ubaguzi wa kijinsia nchini Uhispania, uliochochewa na rais wa zamani wa FA wa Uhispania Luis Rubiales akimbusu mshindi wa Kombe la Dunia Jenni Hermoso kwenye midomo.