Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amepiga marufuku kwa abiria yoyote anayeingia na kutoka Mkoani humo kuingia kwenye usafiri wa umma bila kuvaa barakoa.
Mwanri ametoa maagizo hayo kwenye kikao kazi kilichokutanisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Waganga Wakuu kutathmini mwenendo na udhibiti wa maambukizi ya Virusi vya Corona “Mtu anasema Corona oyee tutakuzibua sisi tunakuja na kitu kinaitwa kubamiza Corona”.