Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu amesema anatafuta vibali vya kukamatwa kwa viongozi wa Israel akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusiana na vitendo vyao wakati wa vita vya miezi saba vya Israel dhidi ya Gaza.
Karim Khan alisema Jumatatu kwamba anaamini Netanyahu, na Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant wanahusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.
Mwendesha mashtaka lazima aombe vibali kutoka kwa jopo la kabla ya kesi la majaji watatu, ambao huchukua wastani wa miezi miwili kuzingatia ushahidi na kuamua ikiwa kesi inaweza kusonga mbele.
Israel si mwanachama wa mahakama hiyo, na hata kama vibali vya kukamatwa vitatolewa, Netanyahu na Gallant hawakabiliwi na hatari yoyote ya mara moja ya kushtakiwa.
Lakini tangazo la Khan linazidisha kutengwa kwa Israeli wakati inasonga mbele na vita vyake, na tishio la kukamatwa linaweza kufanya iwe vigumu kwa viongozi wa Israeli kusafiri nje ya nchi.