Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametoa maagizo ya Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mkuu wa Wilaya ya Same na Mkurugenzi wake kuhakikisha ndani ya muda mfupi wanakamilisha taratibu zote na kufungua soko la Vijana kuanza kutumika na sio kubaki wazi na kuepelekea kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali zinazotokana na kodi za Wananchi.
Makonda ameyasema hayo keo tarehe 22 Januari, 2024 mara baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi wa Same ya kutotumika kwa soko hilo angali ujenzi umeshakamilika.
Naye, Mkurugenzi wa Same amemueleza Mwenezi Makonda kuwa eneo la Soko hilo lilitolewa na Wananchi na kujengwa kwaajili ya Vijana waliochukua mikopo ya halmshauri soko ambalo limejengwa pia kwa ufadhili wa TAA.
Katika hatua nyingine, Mwenezi Makonda ameshauri kwa Wakurugenzi wa Halmashauri Same kusogeza huduma kwenye maeneo tofauti tofauti katika jamii ili kuepukana na mlundikano wa watu na foleni katika kufata mahitaji yao mbalimbali.