Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi amewataka wanandoa kutowaingiza watoto kwenye migogoro ya ndoa kwani kufanya hivyo kunaongeza chuki kwa watoto.
Mwenezi Makonda wakati akisikiliza changamoto ya Mama mmoja mkazi wa jijini Mbeya,amesema ni muhimu kumaliza migogoro hiyo bila kuhusisha watoto na kusema tabia hiyo hutengeneza mioyo migumu kwa watoto pamoja na visasi.
Wakati huohuo Mwenezi Makonda amemtaka Mkuu wa Polisi ya Mbeya kufuatilia mgogoro huo uliozuka baada ya Aliyekuwa mume wa Mama mlalamikaji kudaiwa kwenda kubomo nyumba waliyokuwa wakiishi awali kabla ya kuachana.
Aidha Mwenezi Makonda pia amemuomba Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya kumsomesha mtoto aliyelalamika na kuomba msaada baada ya baba yake kuibomoa nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja kama familia.