Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda wachangia Wazee wauza kahawa na Wanawake Mama ntilie wa eneo la Pongwe kiasi cha Tsh Milioni 2,000,000/= kujiendeleza katika biashara zao.
Pia , amewezesha upatikanaji wa Tsh Milioni 2,200,000/= zilizotolewa na Waziri Ummy (laki 5) Waziri Aweso (laki 5) MNEC – Ndg. Salim (Ratco) aliyechangia (Laki 5) Mwenyekiti wa CCM (M) Tanga Ndugu. Rajabu (Laki 5) pamoja na Kiasi cha Laki 2 kutoka kwa Diwani wa Pogwe katika kuwawezesha Wajasiriamali hao.
Akizungumza na Wajasiriamali hao, Mwenezi Makona amesema wapo watu wanafanya kazi kunwa sana ya kuuza kahawa, mama ntilir na usafirishaji wa bodaboda na CCM na nyinyi ni watu wamoja, hatuwezi kukaa kwenye maofisi ya magari tuu kwasababu nyinyi ndio mnaotuheshimisha kwa kutupa kura nyingi na kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali inayotokana na CCM ikiongozwa na Mwenyekiti Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Najua wengi mna mikopo wengine bado mtaji ni mdogo hivyo nami nimeona ni vema kuwachangia hapa ilikusudi kujiendeleza kwenye biashara zenu, nitawachangia kiasi cha Tsh Milioni 2 mgawane na pesa hii si kutoka kwangu bali ni Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wetu na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwasababu hapa kuna wabunge wenu na Viongozi wa Chama hivyo na wao wameona ni vema kuwaongezea”.