Katibu wa NEC itikadi,uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Makonda ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Ivumwe jijini Mbeya.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo la msingi,Mwenezi Makonda amesisitiza kuhusu kuwalea watoto katika misingi ya maadili,akizitaka zaidi shule zinazomilikuwa na jumuiya ya wazazi wa CCM kuwa za mfano kwenye malezi ya watoto kimaadili.
Aidha jumuiya ya wazazi nchini imetangaza kuzifanyia mapitio shule zote za jumuiya hiyo ili kuendana na mazingira ya sasa na kukudhi mahitaji ya kijamii na mahitaji ya soko la ajira duniani.