Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Makonda amezuru kaburi la Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa.
Mwenezi Makonda aliyesitisha ziara yake mkoani Mtwara kufuatia kifo cha Waziri Mkuu mstaafu Hayati Edward Lowassa ameshiriki pia kwenye sala maalum ya kumuombea kheri na pumziko jema.
Akizungumza na wanafamilia wa Mkapa, Mwenezi Makonda amesisitiza kuhusu uadilifu,mapenzi mema kwa nchi yake na uchapakazi wa Hayati Mkapa kama miongoni mwa tunu muhimu alizokuwa nazo hayati Mkapa.
Hayati Mkapa alizaliwa mwaka 1938 mjini Ndanda na alihudumu nafasi ya Urais wa Tanzania katika kipindi cha 1995-2005 na atakumbukwa kwa uadilifu, uchapakazi na umahiri katika hatua zake za upatanishi na uanzishaji wa taasisi na mashirika mengi ya umma.