Mwenge wa uhuru umepokelewa wilayani muheza na ambapo umefungua,kuzindua,kukagua na kuweka jiwe la msingi kwa miradi nane yenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6 ikihusisha miradi ya Afya,barabara,Elimu,pamoja na utunzajj wa mazingira.
Akitoa taarifa ya kutembelea miradi hiyo mkuu wa wilaya ya muheza Juma Irando amesema kuwa miradi hiyo imehusisha nguvu za serikali pamoja na wananchi na hivyo kukamilika kwake itasaidia kutatua changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zina wakabili wananchi kwenye maeneo yao.
Aidha mbunge wa jimbo la Muheza na waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamisi Mwijuma katika mradi wa barabara amesema kuwa mradi wa ujenzi wa daraja utasaidia kutatua changamoto ya muda mrefu ya mawasiliano katika kuunganisha vijiji vitatu ya Zeneti,Bwiti na Kimbo na hivyo kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.
“Kwakweli tuna mahukuru sana Mhe.Rais kwani kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake ameweza kutupatia fedha Tsh.milioni 30.9 ya ujenzi wa daraja hilo”
Kwaupande kiongozi wa mbilio za Mwenge kiataifa Abdala Shaib Kaim amepongeza ujenzi wa daraja hilo kwani nia ya seriali ni kutatua changamoto ya wananchi wake na kuwaletea maendeleo.
Hata hivyo kauli mbiu ya mbio za mwenge ni “Tunza mazingira Mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa