Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 umekamilisha mbio zake Wilayani Simanjiro ambapo umeona, kuweka mawe ya msingi na kuzindua jumla ya miradi 9, ikiwemo Afya,elimu,Maji,barabara pamoja na Mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mfumo wa ikolojia vijijini yenye jumla ya thamani ya shilingi Bilioni 6.5
Miongoni mwa miradi iliyowekewa mawe ya msingi ni ujenzi wa kituo kipya cha afya TANZANITE inayojengwa na serikalj katika mji mdogo wa Mirerani kwa gharama ya shilingi milioni 500 pamoja na ujenzi wa Barabara ya Sokoni Mirerani hadi Mgodini Tanzanite inayojengwa na serikali kupitia wakala wa Barabara za mijini na vijijini TARURA
Ukiwa katika mji huo wa mirerani mwenge wa uhuru pia umetembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu kinachosimamiwa na shirika la Light in Africa na kukabidhi shilingi milioni mbili taslim kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya kila siku.
Baada ya kukabidhi kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mnzava ametoa wito kwa jamii kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu badala ya kuwaficha kwani serikali imeendelea kuwema mazingira mazuri ya kujjfunzia shuleni..
Ujumbe wa Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 ni “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”