Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Godfrey Mnzava ameipongeza wilaya ya Mkalama kwa kazi kubwa inayofanya katika kusimamia fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa Julai 11,2024 wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru wilaya ya Singida Vijijini mara baada ya kumaliza kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la Msingi katika miradi mitatu iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2024 wilayani Mkalama.
“Tumepita tumeona kazi kubwa imefanyika wilayani Mkalama, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu anatoa fedha lengo likiwa ni kuona wananchi wanapata huduma nzuri. Kazi mnaifanya vizuri, hongereni sana lakini niwaombe tutunze miundombinu vizuri” Mzava
Mbio za Mwenge 2024 wilayani Mkalama zimezindua mradi 1 na kuweka jiwe la msingi katika miradi miwili ambapo miradi yote ina thamani ya jumla ya shilingi 2,067,623,126.00 na umetembelea program 8 ambazo ni Lishe, Mazingira, Rushwa, Dawa za kulevya, VVU/UKIMWI, Malaria, Elimu kwa Mpiga Kura na Kongamano la Vijana.