MWENYEKITI wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Salumu Awadh amesema bodi hiyo inakusudia kuendelea na utaratibu wa kununua mazao kwa wakati katika kipindi ambacho bei ya mazao ipo chini kama sehemu ya mkakati wake wa kuongeza tija kwenye bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na bodi hiyo na hivyo kuwa na nguvu ya ushindani sokoni.
Mwenyekiti wa bodi hiyo ameyasema hayo katika ziara ya siku moja mkoani Iringa kwenye kihenge cha kuhifadhia mazao, na amesema njia pekee ya kujiweka katika mazingira ya kuzalisha bidhaa zenye nguvu ya ushindani sokoni ni kununua mazao ktk kipindi ambacho bei yake iko chini ili kupunguza gharama za uzalishaji.
“ Tunakuwa tunachelewa kununua mazao , kwasababu biashara ya mazao inaendana na muda kwasababu kuna muda unatakiwa ununue yale mazao , lakini ikitokea uzembe kile kipindi cha kununua mazao kikapita , ukaja kununua baadae na hamnunui kwa wakulima mnakuja kununua kwa madalali haita kusaidia wewe kupata faida “ amesema Salum.
Hatahivyo meneja wa Cpb nyanda za juu kusini Jasper Samwel Ametaja baadhi ya shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho ikiwemo uzalishaji wa mahindi na kupata unga katika viwango vizuri na pia kinatoa huduma za uhifadhi wa mahindi pamoja na uzalishaji wa unga .