Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Alhamis Machi 07, 2024, amewasili na kuongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama hicho, huko katika Ukumbi wa Hakainde Hichelema, Jengo la Maalim Seif, Makao Makuu ya ACT- Wazalendo Magomeni Mikumi, Jijini, Dar es Salaam.
Kikao hicho kilichowajumuisha pia wajumbe wapya waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa tarehe 05 na 06 mwezi huu, pamoja na mambo mengine kimejadili ajenda za; Kuthibitisha Uteuzi wa Katibu Mkuu wa Chama na Sekretarieti yake; Kufanya uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu pamoja na Kuthibitisha teuzi nyingine mbali mbali.
Mapema kabla ya kikao hicho cha kwanza tangu kuchaguliwa kwa Uongozi Mpya wa chama hicho hapo jana Machi 06, 2024, katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Othman amehudhuria Kikao cha Kamati ya Uongozi, kilichoongozwa na Kiongozi wa Chama Ndugu Doroth Semu, Katika Ukumbi wa Juma Duni Haji, hapo hapo Makao Makuu ya Chama Magomeni Dar es Salaam
Katika kikao hicho wamehudhuria pia viongozi Wastaafu wakiwemo Kiongozi wa Chama na Mwenyekiti, Ndugu Zitto Kabwe na Juma Duni Haji.