Waziri wa Nishati January Makamba akiwa na Waandishi wa habari amesema kasi ya ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere unaendelea vizuri ambapo ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kinachotosheleza kuzalisha umeme kwenye bwawa la Julius Nyerere.
Waziri Makamba amesema kina Cha bwawa lote lile ni mita 184 kutoka usawa wa Bahari, kina kinachotakiwa kufikiwa ili uanze kuzalisha umeme ni mita 163 kutoka usawa wa Bahari na siku ya Jana imefikia mita 163.61 maana yake kimeshapitiliza kina kinachotakiwa kuzalisha umeme, kuanzia sasa maji yote yanayoingia ni ziada kama na amesema kama ingekua mitambo imemalizwa kufungwa ingeanza kuzungushwa hata leo na maji hayo.
Waziri Makamba aligusia safari yake ya China na kusema ‘Niipoenda Uchina nilienda kutazama na kukagua mitambo yetu itakayofungwa kuzalisha umeme huku Nyumbani na kifaa cha mwisho cha kuzalisha umeme kitaondoka Uchina tarehe 30 Novemba mwaka huu, kwa hiyo bado tuko kwenye ratiba yetu ile ile’ – Makamba.
Kuhusu Ujazo wa bwawa la Julius Nyerere Makamba amesema ujazo ni mita za ujazo Bilioni 30 Hadi kufikia Juzi (July 04 2023) maji yaliyoingia ndani ya Bwawa ni mita za ujazo Bilioni 13.8 ambao ni sawa na asilimia 43.