Kwa mujibu wa tafiti zilizoendeshwa na shirika la afya duniani WHO, kila siku idadi ya watu wanaoambukizwa magonjwa mbalimbali yanayoenezwa kwa njia ya kujamiiana ni milioni moja.Hiyo inamaanisha kuwa zaidi ya maambukizi mapya Milioni 376 kutokea kila mwaka.
Miongoni mwa magonjwa hayo ya zinaa ni kisonono, kaswende, chlamydia, trichomoniasis na ukimwi.
Kwa mujibu wa shirika hilo la afya ukosefu wa ufanisi katika kuzuia kuenea kwa magonjwa ya zinaa ni moja ya sababu za kuenea kwa kasi na kuongeza kuwa kiwango cha maambukizi.
Hatua za dharura za kukabiliana na maambukizi zisipochukuliwa waataalamu wanahofu juu ya kuongezeka zaidi kwa magonjwa ya zinaa na vile vile magonjwa haya kuwa sugu kiasi cha kutotibiwa na dawa zilizopo hivi sasa.
RC GAGUTI ALIVYOONGOZA USIKILIZWAJI KERO ZA ARDHI KATIKA FAMILIA