Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Nchemba, amewaonya baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwenye zoezi la sensa na kupelekea Serikali kushindwa kupeleka huduma za kijamii zinazoendana na idadi ya watu wa eneo husika.
Dr Nchemba amesema hayo Mkoani Manyara katika kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya watu ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Manyara Wilaya ya Hanang’ ambapo amesema Serikali imejipanga kuhakikisha maandalizi ya sensa ya watu na Makazi yanakamilika ili watu wote waweze kuhesabiwa.
Kwa upande wake kamisaa wa sensa ya watu na makazi Bi Anna Makinda, amewataka viongozi wa mkoa wa manyara kuhakikisha wanaelimisha Jamii juu ya umuhimu wa sensa ya watu na mMkazi.
Nae Mbunge wa Jimbo hilo la Hanang’ Mhandisi Samwel Hhayuma ameiomba serikali kuiweka kwenye mipango Ujenzi barabara ya Nangwa-Kondoa ambayo itapunguza kuzunguka umbali mrefu wa zaidi ya Km 200 na kwenda kutumia Km 70 kwenda wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma ili kuwasaidia wananchi wa Kondoa na Hanang’ ambao wanatumia barabara hiyo kusafirisha mazao yao.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani Ni dunia ya watu Bilioni 8 kuhimili wakati ujao na fursa ya haki kwa wote shiriki sensa kwa maendeleo endelevu.