Waziri wa fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mfumuko wa bei ulioshuhudiwa kwa siku za hivi karibuni na kusababisha baadhi ya bidhaa kupanda bei mara dufu huenda ukaanza kupungua kutokana na kushuka kwa nishati ya mafuta katika soko la dunia.
Waziri wa fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ameeleza hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Kimataifa wa taasisi ya kuhakikisha uendelevu wa uwekezaji Duniani (MIGA) inayofanya kazi chini ya Benki ya Dunia.
“Utakumbuka mafuta bei zilikua zinapanda sana lakini katika taarifa iliyotoka hivi majuzi mafuta yamepungua japo hayajafika tulipokuwa mwanzo kabisa ila umeona punguzo la zaidi ya Sh. 400 ambalo ni punguzo kubwa” Mwigulu
“Tunaamini kwa jitihada hizi za Rais za kuweka Bilioni 100 kila mwezi bei za mafuta zitaendelea kupungua, bei za mafuta zinapopungua mfuko wa bei nao utapungua tunakoenda, bidhaa mnazoona hapa kati zimepanda ziliitikia kupanda kwa bei za mafuta” Mwigulu
“ Kwakuwa bei za mafuta zimeshuka na za usafirishaji zitashuka tunakokwenda bidhaa na zenyewe zitaitikia nazo zitashuka” Mwigulu