Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki.

“Mimi nasema tu atakayetaka kutukana atukane tu, hata kama nitakosa Rafiki hata mmoja sawa tu lakini lazima niseme ukweli hata Mtu ana ng’ombe Elfu 12 mnataka Bwawa lake lijengwe kwa kodi ya Nesi au Mwalimu?”- Waziri Mwigulu
“Binafsi kama Binadamu na Mimi nachukia kutoza toza Watu, nachukia kumtoza Mtu fedha yake kabisakabisa, niwaombe Mtu ambaye ana maoni tuendelee kuboresha, hatuna sababu ya kugombana Nchi hii ni yetu, fedha ni zetu na sisi wala hatupingani, Mimi nimepewa dhamana tu na Serikali lakini haitufanyi tuwe Watanzania kuliko Watanzania wengine”- Waziri Mwigulu
Kwa taarifa zaidi unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.
WAZIRI MWIGULU AFUNGUKA YA MOYONI “KISA TOZO ETI NIMEAGIZA MABASI 60, SINA BIASHARA HATA YA BAJAJI”