Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameitaka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliochukua fedha za wananchi kwa ajili ya kuuza ajira za serikali.
“Nasema hadharani kiongozi wa umma lazima afanye kila linalowezekana kuwa mfano na kigezo cha tabia njema na kujiepusha na vitendo vitakavyomfanya atiliwe shaka” Dk Mwinyi.
Aidha,Dk Mwinyi amesema kuwa kuanzia sasa kiongozi yoyote atakayekuwa na kesi ya rushwa na kuwa chini ya uangalizi atasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi.